Book details
| Aina | Kitabu |
| Mfumo wa kitabu | Kitabu chenye jarada |
| Mtunzi | Bishop Dr. Josephat Gwajima |
| ISBN | 978-9987-9300-5-0 |
| Product Code | -- |
| idadi ya kurasa | 135 |
| publisher | Mahanaim printing press |
| uzito | 100gm |
| urefu | 200 mm |
| upana | 150 mm |
Maelezo
Shetani kama mkuu wa ulimwengu amemiliki vitu vingi isivyo sawasawa na hawezi kuviachia kama watoto wa Mungu tusipoamua kushindana naye na kumuamuru aachie Baraka na mafanikio ambayo Mungu ameyakusudia katika maisha yetu..
Ufalme wa giza siku zote hupingana na maisha yetu na neno la Mungu linaonyesha wazi kuwa tunapaswa kushindana na shetani na mapepo yake ili tuweze kuishi maisha ya ushindi, imeandalikwa” kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka , juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”Waefeso 6:12
Josephat Gwajima ni Askofu mkuu wa kanisa la Grolry of Christ Tanzania, kanisa lenye maelfu ya watu wanaomwabudu Mungu pamoja. Ni mtumishi wa Mungu ambaye Mungu humtumia sana kuharibu kazi za ibilisi ,Falme za giza na kuweka huru waliofungwa na nguvu za shetani.
Askofu josephat Gwajima amekiandika kitabu hiki kwa uongozi wa Roho Mtakatifu kama mwongozo wa namna ya kushindana na falme za giza .Tunapoomba maombi ya kushindana kupitia kitabu hiki kwa kumaanisha tutakuwa tukishambulia kiini cha matatizo na kumuamrisha shetani aachie kila kinachokuhusu na utapata ushindi mkamilifu . Hakika kupitia maombi haya ya kushindana utakuwa si tu mshindi bali zaidi ya mshindi katika maeneo yote ya maisha yako.
Read More >>>`
KAMA UMEPENDA BIDHAA YA HAPO JUU NATUMAINI PIA UTAPENDA BIDHAA ZA HAPO CHINI